
Dk.Stella Bitanyi amesema mnyama huyo nikama wanyama wengine hivyo akitunzwa na kuandaliwa vizuri hana madhara lakini kama hatatunzwa vizuri nikweli ana wadudu wenye madhara
Katika hatua nyingine Dk.Bitanyi amesema inakadiriwa kwamba kufikia mwaka 2030, watu zaidi ya milioni 10 watakufa kila mwaka kutokana na dawa kushindwa kuwatibu kwani vimelea vya magonjwa vitakuwa vimejenga usugu unaotokana na matumizi holela ya dawa kwa binadamu na mifugo