Ijumaa , 2nd Mei , 2014

Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduizi Dk. Ali Mohamed Shein amewataka watendaji na wenye vyeo kazini kuacha tabia na mtindo wa kubebana kwa watu ambao hawastahili na badala yake watoe haki inayostahili kwa wahusika.

Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi Dkt Ali Mohammed Shein

Dk. Shein ametoa changamoto hiyo mjini Zanzibar wakati akiwahutubia wafanyakazi wa serikali zote mbili katika hotuba yake ya siku ya wafanyakazi duniani hapo jana.

Mapema wakitoa risala yao ya shirikisho la wafanyakazi wametaka haja ya kuheshimiwa mikataba ya kimataifa na haki zao, kutambuliwa na serikali, huku mwenyekiti wa shirikisho hilo Bw. Zaharani Mohamed Nassor akiitaka serikali kupunguza kodi kwa vile zimekuwa nyingi na zinawatesa wafanyakazi.