
Mkurugenzi mtendaji wa chama cha waandishi wa habari wanawake nchini TAMWA Bi. Eda Sanga.
Ripoti hiyo imetolewa Jijini Dar es salaam, na mkurugenzi mtendaji wa chama cha waandishi wa habari wanawake nchini TAMWA Bi. Eda Sanga wakati akizungumza na wadau wa mambo ya usalama barabarani na watumiaji wa barabara nchini.
Amesema chama hicho kwa kushirikiana na WHO na TAWLA wameamua kutoa elimu ya usalama barabarani kuokoa maisha ya watu kwakuwa vifo milioni 1.24 na majeruhi kati ya 20 na 50 milioni vinatokea kila mwaka na asilimia 90 ya hivyo vyote hutokea katika nchi za Afrika.
Chama hicho kimeona kuna umuhimu wa kulivalia njuga suala hilo la usalama barabarani pamoja wadau wengine kwa kuzifanyia marekebisho sheria na kanuni za usalama barabarani ili kuipa nguvu sheria ya usalama barabarani ya mwaka 1973.