Alhamisi , 30th Jul , 2015

Shule ya msingi juhudi wilaya Morogoro imefungwa kwa zaidi ya miezi miwili kutokana na kukosa choo ambapo wazazi wamelazimika kuchangishana na kujenga matundu ya vyoo lakini hadi sasa serikali haijafungua shule hiyo huku wanafunzi wakizagaa mitaani

Afisa Elimu wa mkoa wa Morogoro Bi Wariambora Nkya.

Wakizungumza wazazi na wananchi wa kijiji cha mtego wa simba ilipo shule hiyo wamemlalamikia kuwa baada ya shule kufungwa wamelazimika kuchangishana fedha na kutengeneza matundu ya vyoo 13 lakini hadi sasa shule haijafunguliwa huku walimu wanaonekana wakizagaa mitaani na wakiendelea kupokea mishahara bila kufanya kazi.

Aidha wazazi hao wameongeza kuwa endapo hatua za haraka hazitachukuliwa katika kuwarejesha watoto hao watawahamisha watoto wao endapo serikali haitafungua shule hiyo.

Nae afisa elimu wa wilaya ya Morogoro Bw, Donald Pambe amesema suala hilo ni la kweli na waliifunga shule hiyo kwa ajili ya Wananchi waweze kulipa suala la Ujenzi wa vyoo na Uchangiaji wa Elimu kwa Ujumla katika shule hiyo na nyinginezo ambazo hazina miundo mbinu rafiki ya Kusomea

Pambe ameongeza kuwa ni kweli shule zilifungwa kwa utaratibu kutokana na kukosa matundu ya choo lakini ameahidi kutuma timu yake kufanya ufuatiliaji ili kujiridhia na hali ilivyo sasa ili kuzifungua shule hizo.