Alhamisi , 15th Nov , 2018

Uongozi wa Shule ya Msingi ya Heaven of Peace Academy (HOPAC) umeomba radhi kufuatia kushtumiwa kuunga mkono vitendo vya mapenzi ya Jinsia moja vitendo ambavyo haviungwi mkono na Serikali ya Tanzania.

Sakata la Ushoga.

Kupitia Mtandao wao Shule  hiyo umeandika ujumbe wa kuomba radhi kuwa wakati siku ya maonesho ya Siku ya kimataifa ambapo wanafunzi wake walibeba mabango ambayo yalitafsiriwa kukiuka maadili ya kitanzania.

Uongozi wa shule yetu unaomba radhi, kwa tafsiri iliyotokea wakati wa maonesho ya siku ya kimataifa iliyofanyika novemba 9 mwaka huu na nia yetu haikuwa kuunga mkono, mapenzi ya jinsia moja au kitu chochote kinachohusiana na mapenzi ya jinsia moja

Tafsiri ya picha inayosambaa kupitia mitandao ya kijamii, imepotoshwa na wala haiwasilishi msimamo wa shule yetu, sisi kama taasisi hatutaki kujihusisha na masuala ya kisiasa ila tutahakikisha tutawachukulia hatua waliohusika kupotosha suala hilo.” imesema taarifa hiyo

Kupitia Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia akizungumza na waandishi wa habari Leonard Akwilapo amesema “ni kweli tumeona kwenye mitandao watoto hao wakiwa wameshikilia bendera zikiwa na rangi nyingi nyingi mpaka hata mimi sijajua nini maana yake.

Lakini baada ya kuona hilo, tayari tumetuma timu ya uchunguzi inayoongozwa na Mdhibiti Ubora wa Kanda ya Dar es Salaam, kwa ajili ya uchunguzi zaidi, kisha tutatoa majibu ya nini kilikuwa kinaendelea,” amesema Dk. Akwilapo.