Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Shule zafungwa Tanzania, Michezo, Matamsha n.k

Jumanne , 17th Mar , 2020

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema kuwa Serikali imezifunga shule zote kuanzia awali hadi kidato cha Sita kwa muda wa mwezi mmoja, ikiwa ni hatua za awali za kujikinga na maambukizi ya Virusi vya Corona.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa

Waziri Mkuu ameyabainisha hayo leo Machi 17, 2020, wakati akitoa tamko rasmi la Serikali na kuitaka Wizara ya Mambo ya Ndani kusimamia mipaka yote na kwamba watu wote wanaoingia nchini waingie kupitia mipaka ambayo ni rasmi.

"Tumefunga Shule zote za Awali hadi Kidato cha Sita na zitafungwa kwa muda wa siku 30 kuanzia leo, Wizara itafanya marekebisho ya ratiba ya mtihani wa kidato cha sita, tumesitisha pia michezo yote inayokusanya makundi ya watu kama Ligi Kuu, Michezo yote ya shule, UMISETA, UMITASHUMITA," amesema Waziri Mkuu.

Waziri Mkuu akatoa agizo kwa Wizara ya Afya,"Wizara ya Afya kuhakikisha kwamba vifaa vya kinga ikiwemo vimiminika vya kudhibiti maambukizi (Hand sanitizer) vinapatikana katika maduka yote husika na kwa bei ya kawaida, Serikali itachukua hatua kwa wafanyabiashara ambao wanapandisha bei".

Aidha Waziri Mkuu amewataka Watanzania kuzingatia kanuni za afya zinazotolewa ili kujikinga na ugonjwa huo na kwamba watu waache kutumia mitandao ya kijamii kwa ajili ya upotoshaji wa taarifa za ugonjwa huo.

 

HABARI ZAIDI

Sehemu ya Ardhi iliyoathirika na Mabadiliko ya Tabia Nchi

Hizi hapa sababu za hali ya hewa isiyotarajiwa

Picha za Satelaiti Zikionyesha Mwenendo wa Kimbunga Hidaya

Kimbunga Hidaya chaendelea kutawala eneo la Pwani

Madaktari Bingwa wa Mama Samia Wakiendelea na Upasuaji

Uvimbe wa kilo 5 waondolewa tumboni kwa mwanamke

Rocket Mwashinga, Chifu Mkuu wa Kabila la Wasafwa

Chifu Mwashinga akemea washirikina kutesa watu

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza na Wanahabari na Wadau wengine kwenye Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete, jijini Dodoma leo Mei 03, 2024.

Watendaji serikalini ondoeni ukiritimba - Majaliwa

Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro SACP Alex Mkama, akionesha vitu vilivyokuwa vimeibiwa

Fundi ujenzi mbaroni mauaji ya dada wa kazi

Wahitimu wa Mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa JKT

Wahitimu JKT watakiwa kulinda miradi ya serikali