Ijumaa , 12th Jan , 2018

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imezionya shule zisizo za serikali zinazofukuza au kuwahamisha wanafunzi kwa kigezo cha kutofikia wastani wa ufaulu ambao shule hizo zimejiwekea bila kufuata wastani uliowekwa na serikali.

Wizara hiyo imezitaka shule hizo kuacha kufanya hivyo mara moja, na shule itakayokaidi itachukuliwa hatua za kisheria kwa kufutiwa leseni ya usajili au kufungiwa kabisa mlinzi 

Aidha kupitia waraka wa Elimu Namba 7 wa mwaka 2004, wizara hiyo pia imewataka wazazi ambao watoto wao walikutana na adha hiyo kuwarejesha katika shule hizo ifikapo Januari 20, 2018.

Taarifa ya wizara hiyo imeeleza kuwa inadaiwa wapo waalimu wakuu wa shule za binafasi wanaofikia hatua ya kuwatuhumu wanafunzi hao kwa makosa ya utovu wa nidhamu na kuwaeleza walezi na wazazi kuwahamisha ama warudie darasa.

Wanafunzi ambao wamedaiwa kukutana na sakata hilo ni pamoja na wale wanaofanya mitihani ya darasa la Nne na Kidato cha pili ambao hurudishwa darasa au kidato ilihali wakiwa wamefikisha wastani wa serikali.