Jumapili , 6th Mar , 2022

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Shaka Hamdu Shaka, amewahakikishia Watanzania kwamba chama hicho kitaendelea kuisimamia serikali izidi kuimarisha uhuru wa maoni, misingi ya haki na demokrasia ili kujenga Taifa lenye upendo, umoja, amani na mshikamano wakati wote. 

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Shaka Hamdu Shaka

Shaka amesema kwamba siasa safi inahusisha uzalendo, utu, heshima na kuweka mbele maslahi ya Taifa kuliko chochote ambapo Rais Samia, amekuwa ni kielelezo katika hili na  ameendelea kuthibitisha dhamira yake ya kuijenga Tanzania moja yenye ustawi kwa wananchi wote. 

Aidha, amebainisha kuwa Ibara ya 118 ya Ilani ya uchaguzi ya CCM inaeleza katika kipindi cha miaka mitano ijayo, Chama Cha Mapinduzi kitaendelea kuheshimu na kulinda misingi ya demokrasia na haki za binadamu kwa ajili ya kudumisha umoja, amani na ustawi wa Taifa kwa kuzingatia katiba ya nchi.