Alhamisi , 28th Oct , 2021

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, amesema kuwa wanawake wana mchango muhimu katika masuala ya siasa na kuinua uchumi wa nchi, hivyo haina budi kuwaangalia kwa jicho la pekee na kuwanusuru katika mambo yanayowadidimiza.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan

Kauli hiyo ameitoa hii leo Oktoba 28, 2021, jijini Dar es Salaam, wakati wa uzinduzi wa kitabu kinachoitwa Tanzania Gender Bench Book on Women’s Rights, kilichoandaliwa na chama cha wanasheria na majaji wanawake nchini Tanzania (TAWJA).

"Hata sehemu za kazi unaweza kumuona mwanamke mwenzio kaingia kazini asubuhi uso haukunjuki vizuri ukimuambia moja anakujibu tatu ukimuita chemba ukimuuliza tatizo limetoka nyumbani, kwahiyo unyanyaswaji unafanya wanawake wasi-perform vizuri", amesema Rais Samia

Aidha Rais Samia akasisitiza, "Afadhali wanaume akikereka huko ana njia zingine za kupita akafurahi na akarudi kazini ametulia, lakini sisi hatuna, ni nyumbani kazini, kazini nyumbani, so handle with care sisi ni assets muhimu".