Jumapili , 14th Sep , 2014

Wafanyabiashara wa Soko kuu la Kilombero lilipo Jijini Arusha nchini Tanzania, wamelalamikia uongozi wa soko hilo kwa kutozingatia usafi wa mazingira na kutojenga uzio wa soko hilo licha ya kulipa ushuru kila siku.

Akiongea kwa niaba ya wafanyabiashara wenzake, mfanyabiashara wa chakula Bi. Zainab Muhamedi amesema wanunuzi wa vyakula sokoni hapo wako katika hatari ya kukumbwa na magonjwa ya tumbo kufuatia mitaro ya maji machafu sokoni hapo kuchakaa kiasi cha kusababisha maji kutuama.

Kwa upande wake, mkuu wa masoko katika maspaa ya jiji la Arusha John Luziga amesema swala la ukuta na kero zingine tayari zimefikishwa kwa mkurugenzi na kuwataka wafanyabiashara kuwapa muda wa kuyatekeleza.

Soko la Kilombero ni soko kumbwa linanalegemewa kwa vyakula kutoka mikoani na licha ya kuwa wafanyabishara wake waliwahi kuhamishiwa katika masoko mengi ila bado lina idadi kubwa ya wafanyabiashara ikilinganishwa na masoko mengine ya jiji la Arusha.