Jumatano , 26th Aug , 2020

Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt Hussein Mwinyi leo amechukua fomu ya uteuzi kutoka Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), na kuweka wazi kuwa dhamira iliyomsukuma kugombea nafasi hiyo ni kuwatumikia Wazanzibari.

Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM, Dkt Hussein Mwinyi.

Amesema hayo akiwa anaongea na wananchi wa Zanzibar hii leo Agosti 26, 2020, mara baada ya kuchukua fomu ya uteuzi, ambapo ameahidi kuleta mabadiliko katika sekta ya viwanda, utalii ambayo yatachangia vijana kupata ajira.

"Nimeamua kugombea nafasi hii kwa dhamira moja tu, nayo ni kuwatumikia Wazanzibar, kwahiyo kuweni na matarajio na Inshaallah mwenyezi Mungu akitujalia kwa kushirikiana tutayatimiza", amesema Dkt Mwinyi.

Aidha Dkt Mwinyi amewausia wananchi wote wa Zanzibar, kuhakikisha wanailinda sana amani walionayao kwani hakuna maendeleo yatakauja kisiwani hapo kama hakuna mani.

"sisi sote tuhakikishae tunahubiri amani na kila mmoja ahakikishe anailinda amani bila ya amani hakuna maendeleo ,bila ya amani hata ibada hatutazifanya tuhakikishe tunailinda amani tuliyonayo" amesema Dkt Hussein Mwinyi.