Alhamisi , 8th Nov , 2018

Spika wa Bunge, Job Ndugai amemzuia Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kujibu swali juu ya kuitwa nchini kwake balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini, Roeland van de Geer kwa kile alichokisema swali hilo lilikuwa nje ya uwezo wa Serikali.

Spika wa Bunge, Job Ndugai, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa

Swali hilo liliwasilishwa bungeni na Mbunge Cecil Mwambe wakati wa kipindi cha maswali na majibu kwa Waziri Mkuu ambapo alihoji juu ya wito wa balozi huyo wa Umoja wa Ulaya.

hivi karibuni tulishuhudia balozi wa EU alikuwa ameitwa kwao kujadili mahusiano ya nchi yetu na jumuiya za kimataifa?” Alihoji Mbunge Cecil

Akitoa maelezo ya maswali hayo Spika Ndugai amesema “napata wakati mgumu kupitisha swali lako sasa kama ameitwa nchini kwao unataka Waziri Mkuu ajibu nini, waziri Mkuu tunakushukuru nenda unaweza kwenda kupumzika.”

Ufafanuzi wa wito wake ulitolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dk.Augustine Mahiga ambapo aliweka wazi kuwa balozi huyo hajafukuzwa kama inavyoelezwa bali ameitwa makao makuu ya umoja huo.

''Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini Tanzania, Roeland van de Geer anayetarajia kuondoka leo usiku kwenda makao makuu ya EU hajafukuzwa bali ameitwa na umoja huo kikazi'', ilieleza taarifa ya Waziri Dr.Mahiga.

Taarifa za kufukuzwa kwa balozi Roeland van de Geer zilisambaa usiku wa Ijumaa mitandaoni na kuzua mijadala mbalimbali, jambo ambalo ilipelekea Waziri husika kutolea ufafanuzi.