Jumanne , 4th Apr , 2023

Askari hao watakuwa sehemu ya kikosi cha kanda ya Afrika Mashariki kinachopambana na kundi la waasi la M23. Hii inafikisha idadi ya wanajeshi wa Sudan Kusini nchini humo kufikia zaidi ya 1,000, kwa mujibu wa Waziri wa Ulinzi Jenerali Chol Thon Balok.

Wanajeshi 300 watapelekwa goma  ambapo ni  makao makuu ya kikosi cha mkoa. Nafasi zao zitabadilishwa baada ya mwaka mmoja.

 Jenerali Santino Deng Wol, mkuu wa vikosi vya ulinzi, aliwaambia wanajeshi walioondoka katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Juba kwamba wanakwenda Kongo kwa jina la Sudan Kusini na chini ya bendera yake, waende wakawalinde raia wa DR Kongo, kuheshimu kila mwanaume na mwanamke wa nchi hiyo.

Sudan Kusini ni nchi ya hivi karibuni kujiunga na kikosi cha mataifa saba ya kikanda kilichoundwa mwezi Juni mwaka jana kujaribu kuleta utulivu mashariki mwa DR Congo.