Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Sugu alitetea Jeshi la Magereza

Jumanne , 22nd Mei , 2018

Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi 'Sugu' amelitetea Jeshi la Magereza mbele ya  Bunge  kuwa jeshi hilo lina matatizo makubwa ya kiusafiri jambo ambalo linapelekea wafungwa kupelekwa Mahakamani kwa miguu kitendo ambacho kina hatarisha usalama wa mfungwa na askari kiujumla.

Kauli hiyo ya Sugu imetolewa leo Mei 22, 2018 Bungeni Jijini Dodoma kwenye kikao cha 34 mkutano wa 11 wa Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wakati wa kipindi cha maswali na majibu kwa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

"Pamoja na matatizo waliyokuwa nayo Jeshi la Polisi katika masuala ya vyombo vya usafiri lakini niwahakikishie Jeshi la Magereza lina hali mbaya sana, hawana magari sio tu magari mabovu hawana magari kabisa, kiasi kwamba wanafikia hatua ya kuwapeleka wafungwa ambao wanakesi Mahamani kwa miguu huku wakiwa wamewafunga pingu. Hii ni mbaya sana kwa usalama wa askari magereza pamoja na wale watuhumiwa ambao wamefungwa pingu", amesema Sugu.

Pamoja na hayo, Sugu ameendelea kwa kusema "mtu anatuhumiwa ujambazi halafu anapitishwa mtaani kwa miguu wananchi wanamuona, wanaweza wakamvamia na kumshambulia pamoja na kuhatarisha maisha ya mfungwa".

Kutokana na ushauri huo, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Mwigulu Nchemba akampongeza Mhe. Sugu kwa kusema "nimpongeze Mhe. Sugu kwa kuuliza swali kwa experience, na niseme kwamba yeye ni mshauri mzuri. Tutalizingatia hilo ili tuweke mgao kwenye upande wa Jeshi la Magereza ili kuepuka na tahadhari aliyosema".

HABARI ZAIDI

Madaktari Bingwa wa Mama Samia Wakiendelea na Upasuaji

Uvimbe wa kilo 5 waondolewa tumboni kwa mwanamke

Rocket Mwashinga, Chifu Mkuu wa Kabila la Wasafwa

Chifu Mwashinga akemea washirikina kutesa watu

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza na Wanahabari na Wadau wengine kwenye Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete, jijini Dodoma leo Mei 03, 2024.

Watendaji serikalini ondoeni ukiritimba - Majaliwa

Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro SACP Alex Mkama, akionesha vitu vilivyokuwa vimeibiwa

Fundi ujenzi mbaroni mauaji ya dada wa kazi

Wahitimu wa Mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa JKT

Wahitimu JKT watakiwa kulinda miradi ya serikali

Daktari wa GGML aliyebobea katika magonjwa yatokanayo na kazi, Cretus Karwan akimpatia vipimo mmoja wa wananchi waliotembelea banda la GGML na kupatiwa huduma za awali za upimaji wa afya katika maonesho ya OSHA yanayoendelea jijini Arusha.

Wananchi 200 wapimwa afya maonesho ya OSHA

Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), Tumaini Nyamhoka akipokea zawadi kutoka kwa Ofisa Mwandamizi wa masuala ya jamii na maendeleo ya kiuchumi kutoka GGML, Ruth Mharagi alipotembelea banda la GGML katika maonesho ya afya na usalama mahali pa kazi jijini Arusha.

TUCTA, OSHA wataka kampuni za madini kuiga ubunifu

Mwili wa Boaz Sanga, Mwanafunzi wa CHuo cha SAUTI Mwanza baada ya kupatikana Pembezoni wa Ziwa Viktoria

Mwanafunzi wa SAUTI afariki akijaribu kuogelea