
Afisa wa maji Bonde la Mto Rufiji ambaye alikuwa mgeni rasimi katika hafla fupi ya kilele cha wiki ya maji Mkoani Mbeya, Idrisa Msuya amesema kuwa taasisi za uma zimekuwa zikisita kulipa ankara za maji na kujilimbikizia madeni.
Msuya amesema kuwa mamlaka za maji nchini zimekuwa zikishindwa kutekeleza majukumu yake kwa weledi kutokana na taasisi hizo kutolipa ankara za maji kwa wakati na kusababisha changamoto kutokwamuliwa katika mamlaka ya maji.
Naye mkurugenzi mtendaji wa mamlaka ya Maji Mkoani Mbeya, Mhandisi Simon Shauri amesema kuwa mbali na changamoto ya ukosefu wa pesa kwa ajili ya shughuli za uendeshaji, mamlaka imekuwa ikifanya juhudi za kuhakikisha wananchi wanapata maji kwa kati ya masaa 15 na 24 kwa maeneo yote ja jiji la Mbeya.