Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Brigedia Jenerali John Mbungo
Hayo yamesemwa Brigedia Jenerali Mbungo katika ofisi mpya za Takukuru zilizopo Mpwapwa ambapo amesema kuwa wahusika wote watachukuliwa hatua ikiwamo kufikishwa mahakamani.
Hayo yanajiri baada ya Rais John Magufuli kugundua kuwa si kweli kuwa shilingi milioni 143 zimetumika kujenga ofi si ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa wakati akifungua ofisi za Chamwino Julai 23.
Baada ya siku kadhaa Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Brigedia Jenerali John Mbungo aliwasimamisha watumishi wa taasisi hiyo ili kupisha uchunguzi na aliwataja waliosimamishwa kuwa ni Jarudi Nyakongeza na Adam Mandia.
Wengine ni Fortunatus Ngailo, Mohamed Kichewele, Nathaniel Otieno, Wilhelm Chuwa, Hamisi Masoud, Mbwana Malumbo na Benedict Mabula.