Jumamosi , 24th Oct , 2020

Wafanyabiashara wa nafaka katika soko la Tandale wameiomba Serikali kuharakisha ujenzi wa soko hilo ili kuondokana na ufinyu wa nafasi na adha ya mafuriko pindi mvua zinaponyesha.

Picha ya soko la Tandale

Wafanyabiashara wa soko la Tandale wameiomba Serikali kuharakisha ujenzi wa soko hilo ili kuondokana na ufinyu wa nafasi na adha ya mafuriko pindi mvua zinaponyesha.

Wakizungumza na KURASA hii leo wafanyabiashara hao wamesema kuwa eneo ambalo kwa sasa wanalitumia ni dogo kiasi cha kushindwa kuhifadhi bidhaa nyingi zaidi.

''Mabanda haya yako wazi na tunapata shida wakati wa mvua ikiwemo kuharibika kwa bidhaa,na unaweza kuleta magunia mia moja ya nafaka yakaharibika yote kwa kuingiliwa na maji nyakati za mvua''amezungumza Rashid Ally mmoja wa wafanyabiashara hao.