Jumapili , 5th Jun , 2016

Shirika la umeme nchini TANESCO limebaini uwepo wa gereji bubu inayotumia umeme wa wizi katika eneo la Unga Limited Jijini Arusha.

Akizungumza katika oparesheni ya kusaka wateja wanaotumia umeme bila kulipia Afisa wa TANESCO John Manyama amesema kwamba kukamatwa kwa watu wanaotumia gereji hiyo kunatokana na msaada wa wananchi wema ambao walitoa taarifa kwa shirika hilo.

Mmiliki wa gereji hiyo Bwn. Ludovick Paulo amesema kwamba yeye anafahamu kwamba analipia umeme na kama kuna mtu alikorofisha mita ya TANESCO kiasi cha kutoandika mahesabu yanayotakiwa yeye hafahamu.

Aidha TANESCO kwa kipindi cha miezi sita nchini wamepoteza kiasi cha shilingi bilioni moja kutokana na wizi wa umeme .