
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa.
Prof. Mbarawa amesema hayo wakati akifungua kikao cha wakala wa barabara nchini Tanroads, kilichofanyika mkoani Dodoma, ambapo amesema miundombinu ya baadhi ya magari hususani malori yamekuwa chanzo cha kuharibika barabara.
Waziri Mbarawa amesema pia pamoja na magari hayo kuharibu barabara lakini pia kuna baadhi ya maeneo wakandarasi wamekuwa siyo waaminifu kwa kutengeneza lami kiwango cha chini na kusababisha kuharibika haraka.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Barabara Hajat Hawa Mmanga, ameiomba serikali kuruhusu kiasi cha mapato yanayotokana na makusanyo ya mfuko wa barabara kulipa watumishi ili kuwaongezea motisha wa kazi