Jumatano , 15th Jun , 2016

Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani amewataka Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) kuhakikisha wanajiridhisha na mizani wanazoweka barabarani ili matumizi yake yachukue muda mrefu bila kuharibika.

Ngonyani ameyasema hayo alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Handeni Omary Kigoda aliyetaka kujua ni lini serikali itafunga mizani zenye ubora katika barabara ya Handeni hadi Korogwe na Handeni hadi Mkata.

Akijibu swali hilo Naibu Waziri Ngonyani amesema barabara hizo zipo mizani na kama suala nim kuhusu ubora wa mizani za muda mrefu anaitaka TANROADS nchi nzima kuhakikisha wanaweka mizani za muda mrefu na zenye ubora katika barabara nchini.