Jumatano , 20th Aug , 2014

Serikali ya Tanzania imeonya juu ya kuwepo kwa ongezeko kubwa la magonjwa yasiyoambukiza yanayotokana na kula vyakula vyenye mafuta mengi na hivyo kumsababishia mlaji kupata magonjwa hayo.

Katibu Mkuu ofisi ya Waziri Mkuu Dkt Florence Turuka.

Akizungumza jijini Dar es salaam katika mkutano wa kutathmini hali ya lishe nchini, Katibu mkuu ofisi ya waziri mkuu Florensi Turuka amesema kwa sasa idadi kubwa ya watanzania wanaofika katika mahospitali wameonekana kuwa na magonjwa ya kisukari, presha pamoja na kuwa na uzito mkubwa kutokana na kula vyakula vyenye mafuta mengi.

Amesema licha ya magonjwa hayo pia watanzania hao wameonekana kusumbuliwa na matatizo ya moyo pamoja na shinikizo la damu wakati mwingine kupata kiharusi jambo ambalo amesema kama watanzania hawatabadilisha tabia za mwenendo wa vyakula kuna hatari ya watanzania wengi kuugua maradhi hayo.

Imeelezwa kuwa ili kupunguza magonjwa kama utapiamlo ,kuongeza kinga ya mwili dhidi ya maradhi,kudumaa pamoja na kuondoa uwelewa mdogo wa kufikiri kunakotokana na ukosefu wa protini.

Ushauri huo umetolewa na mkurugenzi wa utafiti kanda ya kaskazini Dr January Mafuru jana katika mkutano wa tathmini ya shughuli za mradi wa usambazaji wa teknolojia za mahindi lishe.

Mafuru ameongeza kuwa kaya ambazo zimeasha anza kutumia mahindi lishe tayari wameanza kunufaika kwa kupunguza magonjwa hayo ambayo yamekuwa tatizo kwa wananchi wengi wa Tanzania.