Jumatano , 20th Sep , 2023

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, amesema serikali imejiandaa kuanzisha vyanzo vipya vya kuzalisha nishati ya umeme ili Tanzania iweze kuwa na vyanzo vingi vya uzalishaji nishati vitakavyokuwa na nishati ya kutosha na kuuza nchi nyingine za nje.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa

Waziri Mkuu ameyasema hayo wakati anafungua kongamano la kimataifa la tano la nishati lenye lengo la kuangalia fursa, changamoto na mikakati katika uzalishaji wake.

"Tunataka tupanue wigo tuone kwenye solar, upepo na njia nyingine ili tuweze kuwa na umeme wa uhakika na wa kutosheleza ikiwezekena kuuza nje ya nchi," amesema Waziri Mkuu

Kwa upande wake Nibu Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Nishati, Doto Biteko amesema wizara inaendeleza mikakati ya muda mfupi na mrefu ili kuhakikisha Tanzania inakuwa na nishati ya kutosha.