Rais wa Chama cha Madaktari wa Afya ya Kinywa na Meno Tanzania (TDA), Dk. Lorna Carneiro na Makamu wake, Dkt. Ambege Mwakatobe
Wakizungumza wakati wa kuadhimisha siku ya aya ya kinywa na meno duniani wananchi hao wameeleza kufurahishwa na huduma hizo ambapo wamesema ni vyema uwepo utaratibu wa kutoa huduma hizo mara tatu kwa mwaka ili wananchi wapate fursa ya kuelewa namna ya kutunza kinywa na meno yao.
Akitoa tarifa ya zoezi la utoaji huduma ya afya ya kinywa na meno katika maeneo mbalimbali ya manispaa ya Morogoro mkuu wa idara ya kinga ya kinywa na meno hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro Dkt. Baraka Nzobo amesema idadi kubwa ya watoto wanakabiliwa na tatizo la ugonjwa wa meno na fizi.
Kwa upande wake rais wa chama cha madaktari wa kinywa na meno Tanzania (TDA ), Dkt. Lorna Carneiro, ameeleza umuhimu wa maadhimisho ya siku ya afya ya kinywa na meno duniani na kusema Watanzania hawana budi kufanya usafi wa mara kwa mara wa kinywa ili kulinda meno yao





