Jumatano , 5th Aug , 2020

Msanii Top In Dar es Salaam TID, ameangua kilio na kusema amehuzunika sana kwa baadhi ya vyama kutumia msemo wake wa 'Ni yeye' kwenye kampeni zao za kisiasa, huku akidai msemo huo ulikuwa ni maalum kwa Rais John Pombe Magufuli tu.

Msanii TID

TID amesema ameumizwa sana na kitendo hicho kwa sababu amekuwa akitumia akili yake na ubunifu wa kufikiria wazo la msemo huo, hivyo anaona kama anadhulumiwa na kutaka haki itendeke juu ya suala hilo.

“Nimehuzinuka sana na nimeona kwenye mitandao ya kijamii kuwa msemo wangu, ushairi wangu na ubunifu wangu unatumika kwenye kampeni za kisiasa bila ya kuwa na mawasiliano yoyote, nataka niseme kitu kimoja ni muda sasa wa usanii wetu utumike kwa usawa, nimehangaika kutumia akili yangu na nguvu ili kuutangaza huu msemo, naomba mnisaidie nimechoka kudhulumiwa” amesema TID.

Baada ya kusema hivyo TID amewa-tag  Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Juliana Shonza, Katibu wa Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole, Mwana Fa , na Cosota chombo ambacho kinasimamia haki miliki za wasanii.