
Aliyekuwa Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji la Tanzania (TBC) Tido Mhando.
Maamuzi hayo ha Mahakama ya kumuachia huru Tido Mhando yametolewa leo Jijini Dar es salaam na Haki Mkazi Kisutu baada kesi ya kigogo huyo kuunguruma kwa zaidi ya mwaka mmoja ambapo Jamhuri ilimtuhumu Tido Muhando kutumia vibaya ofisi yake.
Miongoni mwa makosa ambayo Tido alikuwa akishtakiwa ni manne yalikuwa matumizi mabaya ya madaraka alipokuwa Mkurugenzi wa TBC ikiwemo kuingia mikataba mbalimbali na baadhi ya kampuni kinyume na taratibu za utumishi wa umma.
Kosa jingine alilokuwa akishtakiwa Tido Mhando ni matumizi ni kuisababishia hasara serikali ya zaidi ya shilingi milioni 800 wakati akiwa mtumishi wa shirika hilo la umma.