Alhamisi , 10th Jul , 2014

Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini Tanzania (TMA) imeendelea kutoa tahadhairi kwa wakazi wa ukanda wa Pwani wa bahari ya hindi kufuatia upepo mkali unaovuma kwa kasi ya kilometa 40 kwa saa pamoja na mawimbi ya zaidi ya mita mbili katika bahari hiyo.

Mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya hali ya hewa nchini Tanzania (TMA) Dkt Agnes Kijazi.

Akiongea na East Africa Redio hii leo jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi wa TMA Dkt. Hamza Kabelwa amesema upepo huo unatokana na kuimarika kwa mgandamizo wa hewa kusini mashariki mwa bara la Afrika hali inayosababisha upepo huo kuvuma kutoka kusini na kuelekea kaskazini.

Dkt. Kabelwa amesema mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Lindi, Mtwara pamoja na visiwa vua Unguja na Pemba vichukue tahadhari ikiwa ni pamoja na vyombo vya usafiri majini kutokana na upepo mkali ulioanza Julai 8 na unatarajiwa kuendelea mpaka Julai 12 mwaka huu.