Mkurugenzi wa TMA Dkt Agnes Kijazi
Akitoa utabiri huo Mkurugenzi wa TMA Dkt Agnes Kijazi amesema kutokana na utabiri huo kuna uwezekano wa kutokea kwa athari za uzalishaji wa mazao ya kilimo hivyo wakulima wanashauriwa kupanda mazao yanayostahamili ukame.
Aidha Dkt Kijazi amesema sekta ya mifugo na uvuvi nayo inatarajiwa kuathirika kwa kuwa upatikanaji wa maji kwa ajili ya mifugo utaathirika na kusababisha migogoro baina ya wakulima na wafugaji.

