Jumatano , 20th Jan , 2021

Rais wa Marekani anayemaliza muda wake hii leo Januari 20, 2021, Donald Trump, ametoa msamaha kwa wafungwa 73 na kupunguza adhabu kwa wafungwa wengine 70. Miongoni mwa waliosamehewa ni pamoja na aliyekuwa mshauri wake mkuu Steve Bannon na rapa Lil Wayne.

Donald Trumpa, Rais wa Marekani anayemaliza muda wake leo Januari 20, 2021

Hatua hii ya Trump kutoa msamaha kwa wafungwa huku wengine akiwapunguzia adhabu, anaitelekeza yakiwa yamebaki masaa kadhaa tu ili amkabidhi kiti hicho Rais mteule wa Taifa hilo Joe Biden, zoezi ambalo litafanyika leo Januari 20, 2021, saa 2:00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki.

Lil Wayne, alikuwa akikabiliwa na mashtaka ya kumiliki silaha kinyume na sheria, huku rapa mwenzake Kodak Black, na aliyekuwa Meya wa Detroit Kwame Kilpatrick, wakipunguziwa vifungo vyao.

Kwa upande wa aliyekuwa mshauri wake mkuu, Steve Bannon, yeye alikuwa akikabiliwa na mashtaka ya makosa ya udanganyifu juu ya kampeni ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kujengea ukuta katika mpaka wa Marekani na Mexico.

Katika kampeni hiyo inadaiwa kuwa Bannon alipokea zaidi ya dola milioni 1, ambazo baadhi ya pesa hizo alizitumia kwa matumizi yake binafsi.