Jumanne , 1st Feb , 2022

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limempitisha Dkt, Tulia Ackson, kuwa Spika wa Bunge.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt, Tulia Ackson

Jumla ya wabunge 376 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wamemchagua Dkt. Tulia kwa kura zote 376 na kuwashinda wagombea wenzake nane ambapo hawajapata kura hata moja.

Dkt. Tulia Ackson, amechukua nafasi hiyo baada ya aliyekuwa Spika wa Bunge hilo, Mhe. Job Ndugai kujiuzulu wadhifa huo Januari 6, 2022.