RC Zainab ametoa kauli hiyo katika mjadala uliokuwa unaendeshwa kwa njia ya mtandao (Zoom meeting) uliowakutanisha wakuu wa mikoa ya kusini - Lindi, Ruvuma na Mtwara
Amesema katika nchi nyingi duniani wamekuwa wakitumia tozo katika maendeleo na hata misaada wanayoleta Tanzania inatokana na tozo
"Wenzetu wanaotuletea misaada fedha inayokuja inatokana na tozo ambazo wanatoa, na sisi watanzania tuone sasa ni wakati wa kuchangia serikali yetu ili iweze kutufanyia makubwa" amesema RC Zainab
Aidha ametaja miradi mbalimbali ambayo inatekelezwa kwa fedha za tozo katika mkoa huo ikiwemo miradi ya elimu
"Katika sekta ya elimu tumepokea bilioni 20.3, lakini shilingi bilioni 8.1 zimetokana na tozo na fedha hizo zimejenga vyumba vya madarasa 401 mabweni mawili lakini tumejenga shule mpya za sekondari 11"
Naye mkuu wa mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas ameeleza baadhi ya miradi mbalimbali inayotekelezwa katika mkoa wake ikiwemo ukarabati wa vituo vya afya na fursa mbalimbali zinazopatikana
"Mkoa wa Ruvuma tumepokea bilioni 1.7 kwa ajili ya kujenga na kukarabati vituo vya kutolea huduma za afya, ambapo kati ya hizo bilioni 1.2 zilikuwa kwa ajili ya umaliziaji wa maboma 50 ya zahanati, na milioni 500 ni kwa ajili ya kituo kimoja cha afya"
"Kwa mwaka 2021/2022 mkoa ulitekeleza miradi mbalimbali ya afya, mkoa umepokea kiasi cha bilioni 5.5 ambazo hizi ni fedha zinazotokana na tozo, zimetuwezesha kujenga vituo vya afya 11"
"Eneo kubwa la mkoa wetu linafaa kwa kilimo cha chakula lakini na biashara, ambazo zaidi ya kilometa za mraba 50673 ambazo ni sawa na hekta milioni 4 sawa na asilimia 79 eneo lote la mkoa linafaa kwa kilimo"
"Fura nyingine ni uwekezaji katika ziwa Nyasa, hatujawekeza sana, tunahitaji wawekezaji wenye teknolojia ya kisasa na vifaa, tunatamani samaki wetu wakitoka ziwa Nyasa kila kitu kiwe kimemalizika pale, tusisafirishe malighafi"
Kwa upande wake Kanali Ahmed Ahmed ambaye ni Mkuu wa mkoa wa Mtwara amewakaribisha wawekezaji mbalimbali kwani mkoa huo una fursa mbalimbali za kiuchumi
"Tuna fursa za umwagiliaji katika wilaya zetu, kwa mfano wilaya ya Mtwara pekee ina hekta kama 9050 ambazo zipo katika eneo la Kitere na Maurunga kwa ajili ya kilimo cha mpunga na mboga mboga"
"Tuna kivutio kingine cha kaburi la mtu mrefu duniani, na inasemekana marehemu huyo alikuwa na urefu wa futi nane, na alizikwa miaka ya 1880, ukija utapata historia yake na kuliona kaburi hilo"
"Natoa rai yangu kwa wasafirishaji wa mazao ya Korosho na Ufuta hasa katika mikoa hii ya kusini watumie bandari ya Mtwara kama sehemu ya kusafirisha bidhaa hizo badala ya kupeleka maeneo mengine"
"Kama kuna wawekezaji wanaoweza kuwekeza kwenye sekta ya utengenezaji wa magari ya gesi waje kuwekeza Tanzania, na kwa kweli gesi ni nyingi, Lindi ipo na Mtwara ipo ndani ya bahari na nje ya bahari"

