Jumanne , 17th Mei , 2016

Waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi amesema serikali imeamua kuandaa mkakati wa kukaa kwa pamoja na wizara zinazohusika na masuala ya ardhi ili kutafuta ufumbuzi wa kudumu juu ya hali hiyo.

Wizara ambazo zitaangaliwa ni pamoja na wizara ya ardhi , maliasili na utalii na wizara ya kilimo na uvuvi ili kuweka utaratibu wa namna ya kupitia migogoro ya ardhi .

Waziri Lujuvi ameyasema hayo alipokuwa akitoa majibu ya nyongeza katika swali lililoulizwa na Mbunge wa Mpanda Vijijini Moshi Selemani Kakoso kuhusiana na migogoro ya ardhi hususani wakulima kufukuzwa na kuchomewa nyumba zao katika maeneo yao.

Hata hivyo majibu ya serikali yametolewa pia kwa Mbunge wa Chemba Juma Nkamia aliyetaka kujua ni lini serikali itahangaika na kumaliza tatizo la wakulima na wafugaji katika mkoa wa Dodoma na Wilaya na wafugaji wa Kiteto mkoani Manyara.

''Tutapitia mgogoro mmoja mmoja baada ya mwingine na kutafuta namna ya kuweza kuitatua''Amesisitiza Waziri Lukuvi.

Suala hili pia lilionekana kumgusa Spika wa Bunge Job Ndugai ambaye amesema ingetoka ruhusa ya watu kuambiwa wasimame kuhusu migogoro basi na yeye angekuwamo kwani matatizo haya yanagusa kila mmoja.