Ijumaa , 23rd Jul , 2021

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Dorothy Gwajima, amewakumbusha wananchi wanaoendelea kufanya mzaha juu ya janga la corona kuchukua tahadhari badala ya kulichukulia kwa wepesi jambo hilo.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Dorothy Gwajima

Dkt. Gwajima ameyasema hayo leo akizungumza na waandishi wa habari amesema kuwa si vema kila siku kutoa tahimini za wagonjwa waliokufa na waliopo badala yake kila mwannachi achukue tahadhari ili kunusuru afya na uchumi wa nchi.

“Nawakumbusha wanaoendelea kufanya mzaha na corona, wasifanye mzaha na UVIKO-19 na tusichukulie wa wepesi kuwa wimbi la kwanza na la pili lilipita, mimi nipo na huyu yupo, wapo wenzetu wengi walipita ukabaki wewe kwa kusudi la Mungu,” amesema Dkt. Gwajima. 

“Na hata leo wapo waliopita na jana wapo waliopita, tusichukulie kwa wepesi jamii ya virusi vinavyozunguka inabadilika sana na inatofautiana makali ya kushambulia hivyo tusiipe miili yetu kazi ya ziada,” amesema Dk. Dorothy Gwajima.

Pia Dkt Gwajima, amewataka viongozi kuwa mstari wa mbele kupamabna na UVIKO 19 huku akieeleza kwamba wapo baadhi ya viongozi ambao hawafanyi vizuri katika kuelimisha jamii yao juu ya tatizo hili la corona.

“Wapo baadhi ya viongozi wanopamabana na janga hilo, wapo baadhi ya viongozi ambao wamejitoa kiani hawafanyi vizuri wanakasi ndogo kusimamia kuwasaidia wananchi washinde vita, watu wasifanye mzaha.” amesema Dkt. Gwajima.