Alhamisi , 22nd Feb , 2018

Maaskari nchini wametakiwa kuzingatia maadili ya kazi na kuacha kuwabambikia watu kesi ikiwa ni pamoja na kujiingiza katika vitendo vya rushwa. 

 

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro akiwa katika ziara yake ya kazi Mkoani Tanga na kusema kuwa askari atakayebainika kupokea rushwa na kuwabambikia watu kesi atachukuliwa hatua za nidhamu.

“Ninatembelea vituo vya polisi kukagua majalada ya kesi, kuangalia sababu za kesi kuchelewa. Pia, ninaangalia kama kuna kesi ambazo wahusika wamebambikiwa ili kuyafanyia kazi mambo haya,”  IGP 

Aidha IGP Sirro amesema endapo kama itabainika kama kuna watu wamebambikiwa kesi basi huyo askari aliyefanya hivyo atawajibishwa kulingana na sheria.