Jumanne , 29th Mar , 2016

Jamii na taasisi hapa nchini zimetakiwa kuwajali watu wasiojiweza na wagonjwa waliolazwa hospitalini na wale waliopo majumbani ikiwa ni ishara ya upendo kwao kuwapa faraja.

Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Njombe (Chadema) Lucia Mlowe

Mbunge wa viti maalum mkoa wa Njombe (Chadema) Lucia Mlowe, ameamua kuitumia Fursa ya mapumziko ya sikukuu ya Pasaka kutoa msaada wa vitu mbalimbali vikiwepo vyakula, kwa watu wasio jiweza na wagonjwa mkoani Hapa.

Baadhi ya wananchi na jamii ya mkoa wa Njombe wamesema kuwa pamoja na kumshukuru Mbunge huyo wameziomba taasisi nyingine ziwe na moyo wa kujitolea kwa watu wenye mahitaji maalum.

Aidha Mbunge huyo alipata Nafasi ya kutembelea wanawake, na wazee, wanao ishi katika mazingira magumu na hatarishi katika mitaa ya Mgendela, National housing na hospitali ya Mkoa wa Njombe Kibena.