Ijumaa , 18th Nov , 2022

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax amepongeza uamuzi wa Serikali ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) wa kufungua Konseli Kuu (Ubalozi Mdogo) Visiwani Zanzibar na kutoa wito kwa Wananchi kutumia uwepo wa Konseli hiyo biashara.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax

Mhe. Dkt. Tax ametoa pongezi hizo hivi karibuni wakati akipokea Hati za Utambulisho za Konseli Mkuu wa UAE, Zanzibar Mhe. Balozi Saleh Ahmed Alhemeiri katika hafla fupi iliyofanyika katika Ofisi za Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Zanzibar.

Amesema hatua hiyo ni muhimu sana katika kuimarisha ushirikiano wa kihistoria uliopo kati ya Tanzania na UAE kwani sasa fursa nyingi zilizopo Zanzibar ikiwemo utalii, uchumi wa buluu na biashara vitashamiri zaidi na kukua.