Jumatatu , 5th Dec , 2022

Vyombo vya dola vimetakiwa kufanya uchunguzi wa kina wa kifo cha Askofu mstaafu Boniface Kwangu, wa kanisa la Anglikana Diocese ya Victoria Nyanza, anayedaiwa kupotea tarehe 28 na mwili wake kukutwa ukielea ndani ya maji kandokando ya Ziwa Victoria karibu na linapojengwa daraja la JPM.

Askofu mstaafu Boniface Kwangu, aliyefariki dunia

Kauli hiyo imetolewa na Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Tanzania, Mhimbo Mndolwa, wakati mwili wa Askofu Mstaafu Kwangu ukiagwa ndipo akaomba uchunguzi wa kina ufanyike ili kuwababini waliofanya mauaji hayo ya kutisha

"Tunaiachia serikali kwa wahusika wa kifo cha Askofu Mstaafu Kwangu kama kuna aliyehusika basi sheria ichukue mkondo wake," amesema Askofu Mndolwa

Akisoma risala ya marehemu Askofu Mstaafu Kwangu, Benedict Kwangu, amelishukuru jeshi la polisi kwa kushirikiana na wavuvi wa eneo hilo kuweza kufanikisha kuupata mwili wa Askofu huyo.