Jumatatu , 30th Dec , 2019

Baada ya miezi kadhaa ya mashambulio ya mabomu kutoka kwa vikosi vya Syria na Urusi, Mji wa Kafr Nabl nchini Syria, sasa umebaki kuwa makazi ya Paka wengi, kuliko idadi ya watu iliyopo kwa sasa.

Picha ya Paka.

Watu wachache waliobaki katika mji huo wa Syria, wanajiliwaza na zaidi ya mamia ya Paka, baadhi ya wakaazi hujificha chini ya kifusi cha nyumba zilizobomolewa ili kujikinga dhidi ya mabomu yanayodondoshwa kutoka angani.

Mmoja wao ni Salah Jaar, mwenye umri wa miaka 32, ambapo katika kifusi kilicho karibu naye, kuna mamia ya Paka, ambapo yeye anadai kufarijika pindi wanapokuwa karibu naye.

"Watu wengi wamehama mji wa Kafr Nabl hali iliyofanya idadi ya watu kuwa ndogo sana, kwa kuwa Paka wanahitaji watu wakuwatunza kuwapa maji na chakula, wamehamia katika nyumba za watu walioamua kubaki katika mji huo, kila nyumba ina karibu paka 15, au hata zaidi" amesema Salah.

Aidha Salah ameongeza kuwa, "Kila ninapokula, nao hula, iwe ni maboga,spageti au hata mkate uliokauka, katika hali hii nahisi sote ni viumbe wadhaifu na tunahitaji kusaidiana".

                                         Salah akiwapa Paka chakula.
Chanzo, BBC.