Viongozi hao watatu wamekutana siku ya jana ambapo wote wapo kwenye mkutano wa baraza kuu la umoja wa mataifa huko jijini New York.
Kwa mujibu wa Rais Macron viongozi hao wanataka kumaliza tofauti zao ikiwemo kukomesha vitendo vya waasi.
Waasi wa kundi la M23 wamekua wakitawala eneo la Kaskazini mwa Congo toka mwezi juni.
Katika Mkutano huo ambao Rais Félix Tshisekedi wa Congo aliilaumu Rwanda kwa kuunga mkono waasi wa M23, Rais wa Rwanda alijibu ka kusema kwamba ‘’lawama haziwezi kuleta suluhu’’