Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Ugonjwa wa ajabu waua watu wanane Kenya

Ijumaa , 9th Apr , 2021

Ugonjwa wa ajabu umeua watu wanane kwenye kijiji kidogo kilichoko katika  Kaunti ya Kakamega nchini Kenya.

wakazi wa kijiji cha Shina

Mamlaka husika zilithibitisha vifo katika wadi ya Isukha Magharibi, lakini sababu ya ugonjwa huo bado haijafahamika.

Moja ya dalili ambazo wagonjwa wameeleza kuwa nazo ni pamoja na kutokewa na vipele vinavyowasha ambavyo hupelekea malengelenge na kuvimba kwa mikono, na kusababisha kifo hapo baadae.

Aidha, mmoja wanakijiji alisema hofu ilishika kijiji cha Shina kutokana na  uvumi ulioenea kwamba ugonjwa huo kuhusishwa na imani za kichawi baada ya pombe ya kienyeji kuibwa kutoka nyumbani na mmiliki wa nyumba kutishia kwenda kwa mganga.

Nao wagonwa amabao wanasumbuliwa na ugonjwa huo wamelalamikia maumivu makali wanayoyapata ilihali tiba za asili zikishindwa kusaidia na wengine wakishindwa kwenda hospitali kwa hofu.

“Mume wangu alianza kufanya vitu sio vya kawaida, aliniambia hakuwa mzima na aliogopa angekufa na hata alitishia kujiua kwa sababu ya maumivu,” alisema mjane Violet Wiraka ambaye alishuhudia mumewe akiugua ugonjwa hadi kukumbwa na umauti. 

Kwa upande wake Gavana wa Kaunti ya Kakamega Wycliffe Oparanya amesema wanasubiri ripoti kutoka kwa timu ya wataalum wa afya walioituma ili waweze kukabiliana na hali hiyo kwani bado nchi ipo kwenye wimbi la virusi la corona.

HABARI ZAIDI

Sehemu ya Ardhi iliyoathirika na Mabadiliko ya Tabia Nchi

Hizi hapa sababu za hali ya hewa isiyotarajiwa

Picha za Satelaiti Zikionyesha Mwenendo wa Kimbunga Hidaya

Kimbunga Hidaya chaendelea kutawala eneo la Pwani

Madaktari Bingwa wa Mama Samia Wakiendelea na Upasuaji

Uvimbe wa kilo 5 waondolewa tumboni kwa mwanamke

Rocket Mwashinga, Chifu Mkuu wa Kabila la Wasafwa

Chifu Mwashinga akemea washirikina kutesa watu

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza na Wanahabari na Wadau wengine kwenye Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete, jijini Dodoma leo Mei 03, 2024.

Watendaji serikalini ondoeni ukiritimba - Majaliwa

Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro SACP Alex Mkama, akionesha vitu vilivyokuwa vimeibiwa

Fundi ujenzi mbaroni mauaji ya dada wa kazi