Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Ujenzi bomba la mafuta kutoka Uganda waiva

Jumapili , 26th Feb , 2017

Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni amemhakikishia Rais wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kuwa yupo tayari kuweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga nchini Tanzania.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na mgeni wake Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Terminal 1 kabla ya kuondoka ma kurejea nchini kwake.

Mhe. Rais Museveni amesema hayo leo tarehe 26 Februari, 2017 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam wakati akiagana na mwenyeji wake Mhe. Rais Magufuli baada ya kumaliza ziara yake rasmi ya kiserikali ya siku 2 hapa nchini na kurejea Uganda.

“Tulikuwa na mazungumzo mazuri na Mhe. Rais Magufuli, tumejadili mambo mengi hususani kuhusu mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta, tumekubaliana na Mhe. Rais mambo mengi, na sasa tutakwenda kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa mradi huo” amesema Mhe. Rais Museveni.

 Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpokea Mgeni wake Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Terminal 1 kwa ajili ya kurejea nchini kwake Uganda mara baada ya kumaliza ziara yake ya siku mbili hapa nchini. 

Mhe. Rais Museveni aliwasili hapa nchini jana asubuhi tarehe 25 Februari, 2017 ambapo amefanya mazungumzo na mwenyeji wake Mhe. Rais Magufuli na leo ametembelea viwanda viwili vinavyomilikiwa na kampuni ya mfanyabiashara wa Tanzania Bw. Said Salim Bakhresa ambavyo ni kiwanda cha uzalishaji wa unga wa ngano kilichopo Buguruni na kiwanda cha uzalishaji wa juisi kilichopo Vingunguti Jijini Dar es Salaam.

Licha ya kuwekeza nchini Uganda Mfanyabiashara huyo pia amekuwa akipeleka bidhaa zake kwa wingi nchini Uganda.

Pamoja na Mhe. Rais Magufuli viongozi wengine waliokuwepo wakati wa kumuaga Mhe. Rais Museveni ni pamoja Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa na Viongozi wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama.

 Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akiagana na Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni kabla hajapanda ndege na kurejea nchini kwake Uganda mara baada ya kumaliza ziara yake hapa nchini.

HABARI ZAIDI

Mkuu wa Usalama Barabarani mkoa wa Songwe Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Charles Bukombe, akizungumza na abiria

"Fungeni mikanda muda wapo safarini" - SSP

Mbunge wa Kilosa Profesa Palamagamba Kabudi

"Ndege ijayo ipewe jina la Mwl Nyerere" - Profesa

Baadhi ya Wanachi wa Kata ya Msowero, wakiwa Katika Mkutano wa Hadhara na Mkuu wa Wilaya

Mwenyekiti atiwa mbaroni kwa kuuza mlima, Msowero

Sehemu iliyokumbwa na Mafuriko Kusini mwa Brazil

Wanaokufa kutokana na mafuriko waongezeka Brazil

Baadhi ya Wabunge Wakichangia Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Uchukuzi

Serikali yashauriwa kuwa bunifu sekta ya usafiri

Baadhi ya Wananchi Wakishudia Ajali Iliyomgonga Mwendesha Bodaboda

Watatu wanusurika kifo, scania ikimgonga bodaboda