Ijumaa , 27th Nov , 2020

Katika siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia, Mwanaharakati, kutoka Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, (LHRC), Joram Bwire, amesema kuwa yapo mambo madogo madogo ambayo inabidi yafanyiwe kazi ili kutomekeza ukatili wa kijinsia ikiwemo maboresho ya kamati zilizoundwa.

Pichani:Mfano wa mtu aliyefanyiwa kitendo cha ukatili

Akizungumza katika kipindi cha Supa breakfast, cha East Africa Radio, Joram Bwire amesema licha ya ukatili wa kijinsia kuonekana unazidi kushika kasi serikali imefanya juhudi mbalimbali kuhakikisha inaondoa tatizo hilo.

“Kuna mambo madogo madogo inabidi yafanyike kwamba hizi kamati inabidi ziboreshwe kwa kujengewa uwezo ili kurahisisha utendaji kazi” amesema

Aidha Bwire akizungumzia ukatili wa ukeketaji amesema kuwa katika kuhakikisha tatizo hilo linatatuliwa lazima chanzo chake kijulikane ili liweze kutatauliwa huku akisema kuwa  tatizo hili limechukua sura mpya ambapo watoto ufanyiwa ukeketaji mara tu wanapozaliwa hospitalini hivyo kuwalazimu kuweka ulinzi shirikishi hospitalini kwa ajili ya kudhibiti tatizo hilo.