Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

"Ukikamatwa hautapata dhamana" - Jerry Muro

Jumapili , 21st Apr , 2019

Mkuu wa wilaya ya Arumeru, Jerry Muro ametoa onyo kali kwa watu wenye tabia za ubakaji na udhalilishaji wa kingono kwa watoto na wanawake, na kusema kwamba kwamba kwenye wilaya yake iwapo mtu atakamatwa hatopewa dhamana.

Akizungumzia hilo mbele ya umati uliokuwa ukimsikiliza mapema leo, Jerry Muro amesema kwamba mtu yeyote atakayekamatwa kwa makosa ya ubakaji na udhalilishaji wa kingono, ajue wazi kuwa hatopata dhamana akiwa kituoni, labda iwe mbele ya mahakama.

Jerry Muro ameyasema haya

 

“Watu wenye vitendo vya ubakaji na udhalilishaji kwa watoto, wanawake na kina mama, katika Wilaya yetu huna dhamana, utakapopelekwa kituo cha polisi, tunajua dhamana ni haki yako, lakini katika hili Arumeru tumejiwekea utaratibu, hautapata dhamana, utashikiliwa mpaka kesi itakapokwisha, polisi huku tutakushikilia, hautapewa dhamana kituo cha polisi, omba Mungu ukapewe dhamana mahakamani kama utapelekwa mahakamani ukapewa dhamana mahakamani”, amesema Jerry Muro

Akiendelea kuzungumzia hayo Jerry Muro amesema kwamba iwapo atalalamikiwa kukiuka kwa haki za binadamu kwa kumnyima dhamana mbakaji, ni vyema wakajiuliza iwapo haki hizo zinaruhusu kufanya maovu hayo, na iwapo hairuhusu basi wajue wazi kuwa hata wao hakli yao ya dhamana haitapatikana.

Hatufanyi hii kukiuka haki za binadamu, hakuna haki za binadamu inayoruhusu mtu mzima kumuingilia mtoto mdogo, kwa hiyo usitafute haki za binadamu wakati nimesha kukamata, kabla hujatafuta haki za binadamu, jiulize kwanza kabla ya kwenda kubaka mtoto, je haki za binadamu zinaruhusu kwenda kubaka mtoto, kama haziruhusu kubaka mtoto haki hizo hizo za binaadam hazitaruhusu mimi kukupa dhamana”, amesema Jerry Muro.

Jerry Muro pia amezidi kuwasisitiza vijana waendesha boda boda wa ndani ya mkoa huo kujiepusha na vitendo hivyo, kwani wamekuwa wakisifika kwa kufanya maovu kumalizia 'handasi' zao kama alivyoitaja.

HABARI ZAIDI

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda (Mwenye shati ya Bluu) akipata maelekezo wakati wa maonesho ya OSHA 2024 kwenye Viwanja vya General Tyres jijini Arusha.

RC ataka GGML iboreshe maisha ya wananchi Geita

Vijana Waliojiajiri Sekta ya Kilimo, Nigeria

Mishahara yaongezeka nchini Nigeria

Coaster iliyoparamia nyumba Bukoba

Tisa wanusurika kifo Kagera

Picha ya Fat Joe na Chris Brown

"Chris Brown anafaa kuwa 2Pac wa kisasa" - Fat Joe

Katibu wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Amani Golugwa

Maandamano yetu sio kelele za wahuni - Golugwa