Alhamisi , 13th Oct , 2016

Serikali imeanza kufanya utafiti wa kuangalia hali ya upatikanaji wa nishati Tanzania hususani katika maeneo ya vijijini kwa mwka 2016.

Kazi ya usambazaji wa nguzo za umeme vijijini

Tathmini ya awali inaonesha kuwa upatikanaji wa umeme vijijini umeongezeka kutoka 2% mwaka 2007 hadi 41% mwaka huu.

Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa wakala wa Nishati Vijijini (REA) Mhandisi Gissima Nyamo-Hanga wakati akizungumzia uanzishwaji wa utafiti wa kuangalia hali ya upatikanaji wa nishati Tanzania wa mwaka 2016.

Utafiti huo unafanyika mikoa yote 26 ya Tanzania bara kati ya tarehe 10 Oktoba na tarehe 15 Novemba 2016 kwa muda wa siku 25.Utafiti huu unafanywa na serikali kupitia wakala wa nishati vijijini REA pamoja na ofisi ya Taifa ya Takwimu.

Lengo la utafiti huo ni kukusanya takwimu rasmi zinazohusu hali ya upatikanaji wa nishati ya umeme katika ngazi ya jumuiya na kaya, matumizi ya umeme na nishati jadidifu pamoja na faida zake kwa maendeleo.

Utafiti huo utahusish jumla ya maeneo 676 ya vijiji na mijini yaliyochaguliwa kitaalam katika mikoa yote 26 ya Tanzania Bara na utahusisha jumla ya kaya binafsi zipatazo 10,240 pamoja na viongozi wa vijiji na mitaa 676 ambao watahojiwa kuhusu miradi mbalimbali ya maendelei inayopatikana katika maeneo yao.

Timu ya Wadadisi wapatao 130 watahusika katika ikusanyaji wa taarifa hizo ambapo kila mkoa utakuwa na wadadisi watano, msimamizi mmoja na wataalam wengine kutoka ofisi ya taifa ya takwimu makao makuu.