Jumanne , 18th Oct , 2016

Umoja wa Mataifa nchini Tanzania umeitaka serikali kuwashirikisha vijana katika utekelezaji wa Malengo Endelevu ya Maendeleo, SDG, kwani vijana ni 70% ya nguvu kazi ya taifa, ambao wakijengewa uwezo watachangia kikamilifu kwenye uchumi wa nchi.

Vijana wa kitanzania katika shughuli zao

Mtaalam wa ajira kwa vijana kutoka Shirika la Kazi Duniani, ILO, Bi. Annamarie Kiaga, amesema, kutowashirikisha vijana kutachelewesha maendeleo yao na taifa kwa ujumla hivyo ni vyema ikaundwa sera ya namna ya kuwashirikisha na kujitegemea.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Michezo na Sanaa, Profesa Elisante Ole Gabriel, amesema ni vyema vijana wakajenga tabia na mitazamo ya kujitegemea ki-fikra bila kusukumwa kwani serikali inathamini mchango wao katika kuleta mabadiliko chanya baina yao na jamii kwa jumla.