Utaratibu wa kuingia getini, maonesho ya Sabasaba

Jumanne , 30th Jun , 2020

Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaniva amezitaka Taasisi za Serikali na za binafsi kufanya ujenzi wa mabanda yao usiku na mchana ili kukamilisha na kuanza kutoa huduma kuelekea maonesho ya Sabasaba.

Eneo la maonesho ya Sabasaba Jijini Dar es Salaam

Ametoa rai hiyo mara baada ya kufanya ukaguzi katika viwanja vya maonesho ya 44 ya biashara SabaSaba ambapo pia amepata nafasi ya kuzindua kadi maalum itakayotumika katika maonesho hayo kwenye kuingia magetini na hata kwenye manunuzi ya bidhaaa mbalimbali endapo mwananchi atavutiwa kufanya hivyo.

Akiwa katika ziara hiyo ya kukagua mabanda mbalimbali likaibuka sakata la wananchi wajasiriamali ambao wamedai kuwepo kwa  ubaguzi katika utolewaji wa mabanda.

Maonesho hayo ya SabaSaba yanatarajiwa kuanza Julai Mosi na kuhitimishwa Julai 13 yakihusisha ushiriki wa mataifa mbalimbali ambapo Watanzania wameaswa kutumia fursa hiyo kukua kiuchumi.