Jumamosi , 3rd Jun , 2017

Mbunge wa Arusha mjini, Mh. Godbless Jonathan Lema amedai Vyombo vya usalama vimezuia kuaga mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Moshi mjini Mh. Philemon Ndesamburo kwenye uwanja wa Mashujaa.

Mbunge wa Arusha mjini. Mh. Godbless Lema

Kupitia ukurasa wake wa twitter Mh. Lema amedai kuwa amezungumza na Diwani wa kata ya Sombetini Mh. Ally Bananga na kwamba wamezuiliwa na vyombo vya usalama kufanyia hapo shughuli ya kumuaga Mzee Ndesamburo.

"Nimeongea na Mh Bananga aliyeko uwanja wa mashujaa , vyombo vya usalama vinazuia kuaga mwili wa Ndesamburo kuagwa hapo. Hii ni mbaya sana" - Mh. Godbless Lema.

Ujumbe wa Mh Lema kupitia ukurasa wake.