Jumatatu , 29th Feb , 2016

Vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), vimesema vinaelekea kuishiwa uvumilivu wa kisiasa kutokana na kupuuzwa kwa maamuzi ya wananchi mara kwa mara ikiwemo kwenye chaguzic mbalimbali.

MWENYEKITI Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ambaye pia ni mwenza wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananachi (UKAWA), Freeman Mbowe

Mwenyekiti wa Umoja huo Freeman Mbowe Mbowe amesema hayo kwenye Ibada ya Kuchangia kwenye kanisa la KKKT ,Nshara Wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro na kuongeza kuwa suala la Uchaguzi wa Zanzibar na kusuasua kwa uchaguzi wa Meya wa Jiji la Dar es Salaam, ni vielelezo vya serikali kupora demokrasia.

Aidha Mwenyekiti huyo Mwenza wa Umoja huo, amesema kuwa uvumilivu una mwisho hivyo ameitaka serikali kuacha kutumia nguvu katika masuala ya kuwatumikia wananchi na kuwapa uhuru wa maamuzi wanayoyataka.

Mhe. Mbowe amesema kuwa Chama cha Mapinduzi kimeonyesha kushindwa katika chaguzi kadhaa lakini kinalazimisha kuendelea kushikilia madaraka kwa nguvu hasa kwenye chaguzi za Mameya ikiwemo Uchaguzi wa Meya wa Jiji la Dar es Salaam.