Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga, George Kyando
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga, George Kyando, akizungumza na waandishi wa habari mkoani humo amesema kuwa atahakikisha changamoto ya vibaka kuvamia mitaani inakwisha na wananchi wanaishi kwa amani, huku akiwataka waendesha bodaboda kufuata sheria ili kuepusha ajali za barabarani.
Wakizungumzia changamoto ya vibaka baadhi ya wakazi wa Manispaa ya Shinyanga wakalitaka Jeshi la Polisi kuendelea kuimarisha ulinzi ili kukomesha matukio hayo.





