Alhamisi , 10th Nov , 2022

Wizara ya Ardhi imesitisha kutoka vibali vipya vya ujenzi wa vituo vya mafuta na mabadiliko ya matumizi ya ardhi kwa ajili ya vituo vya mafuta kwa muda wa miezi mitatu 3 kuanzia leo Novemba 1o, 2022, ili kutoa nafasi kwa Wizara zinazohusika na utoaji wa vibali kufanya tathmini ya kina.

Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk.Angeline Mabula

Agizo hilo limetolewa na Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk.Angeline Mabula, mara baada ya ongezeko la ujenzi holela wa vituo vya mafuta visivyozingatia matakwa ya sheria ya mipangomiji na kanuni zake.

Katika hatua nyingine Dk.Mabula amesitisha kutoa vibali vipya vya ujenzi vinavyokiuka mipango kabambe wa Majiji, Manispaa ,Miji na kusitisha ugawaji viwanja kiholela unaopelekea taswira ya miji na kusitisha ugawaji viwanja kiholela unaopelekea taswira ya miji kuharibika.