Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Video: Kufuga wahalifu kuna gharama

Jumapili , 21st Mei , 2017

Waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mhe.Mwigulu Nchemba amewaonya wananchi wa Kibiti mkoa wa Pwani kutowaficha wahalifu wanaofanya mauaji mkoani humo bali wawafichue ila maisha yaweze kuendelea kama zamani na kudai pasipo kufanya hivyo kuna gharama.

Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba

Mhe. Mwigulu amewataka wananchi kutambua kwamba kuendelea kuwaficha wahalifu waliopo ndani ya jamii watambue kuna gharama kubwa ambayo itawafanya maisha yasiweze kusonga mbele.

Mwigulu ameyasema hayo leo Kata ya Bungu wilaya ya Kibiti mkoa wa Pwani mara baada yakutembelea majeruhi na kambi maalum ya jeshi la Polisi mkoani humo kwa ajili ya kupambana na waalifu ambao wanajihusisha na kuua wananchi ,viongozi wa dini na vyama.

Wakati akizungumza na wananchi pamoja na kikosi maalumu kilichopo huko, Mhe. Mwigulu amesema kwamba serikali imejipanga vyema kubana mianya ya wote wanaofanya mauaji hayo na kuongeza kwamba itawatia nguvuni, na kuwataka wananchi kuwa mstari wa mbele kuwafichua wahalifu hao

Nchemba ameendelea kufunguka kwamba  uhalifu unaoendelea kwa sasa maeneo hayo ya Kibiti yanasababisha wasiwasi kwa wananchi na kuongeza kuwa serikali haitawaacha wahalifu  waendelee kufanya mauaji hayo na kuongeza kwamba hakuna ruhusa ya aina yeyote ya mtu kumuua mwenzake kwa misingi yakua na mtazamo tofauti wa dini, chama , kabila na asili.

Pamoja na hayo ameongeza kwamba serikali imeanza kuwabaini wahusika wa vitendo hivyo na bado wanaendelea na uchunguzi ili kuwabaini wahalifu wengine.

HABARI ZAIDI

Sehemu ya Ardhi iliyoathirika na Mabadiliko ya Tabia Nchi

Hizi hapa sababu za hali ya hewa isiyotarajiwa

Picha za Satelaiti Zikionyesha Mwenendo wa Kimbunga Hidaya

Kimbunga Hidaya chaendelea kutawala eneo la Pwani

Madaktari Bingwa wa Mama Samia Wakiendelea na Upasuaji

Uvimbe wa kilo 5 waondolewa tumboni kwa mwanamke

Rocket Mwashinga, Chifu Mkuu wa Kabila la Wasafwa

Chifu Mwashinga akemea washirikina kutesa watu

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza na Wanahabari na Wadau wengine kwenye Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete, jijini Dodoma leo Mei 03, 2024.

Watendaji serikalini ondoeni ukiritimba - Majaliwa

Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro SACP Alex Mkama, akionesha vitu vilivyokuwa vimeibiwa

Fundi ujenzi mbaroni mauaji ya dada wa kazi

Wahitimu wa Mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa JKT

Wahitimu JKT watakiwa kulinda miradi ya serikali